Gomes Aichimba Mkwara Yanga-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Gomes Aichimba Mkwara Yanga-Michezoni leo

WAKATI Yanga ikibainisha kwamba inahitaji kusepa na taji la Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2021/22 lililo mikononi mwa Simba, Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes amewachimba mkwara kiaina kuhusu taji hilo.

Juzi Simba ilikuwa na kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao ulihezwa nchini Botswana na Simba kuibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Jwaneng Galaxy.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Gomes alisema kuwa wanatambua ligi ya msimu wa 2021/22 ni ngumu ila uhitaji wao ni kutwaa ubingwa kwa kuwa ipo kwenye hesabu zao.

“Tunajua kwamba ligi ni ngumu na kila timu inapambana kupata ushindi hilo halitupi tabu kwani malengo yetu yapo palepale ni kuona kwamba tunashinda taji la ligi ambalo lipo mikononi mwetu.

“Ukiwatazama wachezaji ambao wapo wote wapo tayari na nguvu ipo kwetu kuweza kufanya vizuri, kila kitu ni mipango na tuna amini kwamba tutafanikiwa,” alisema Gomes.

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam

The post Gomes Aichimba Mkwara Yanga appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz