Gomes Aanza Kupambana na Sakho Simba SC-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Gomes Aanza Kupambana na Sakho Simba SC-Michezoni leo

KIUNGO mshambuliaji mpya wa Simba, Ousmane Pape Sakho amerejea mazoezini pamoja na wachezaji wenzake baada ya kupona jeraha la mguu huku akipewa mazoezi maalum ya fitinesi.

 

Kiungo huyo ni kati ya wachezaji waliosajiliwa na timu hiyo katika kujiimarisha na Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu Bara.

 

Nyota huyo alikuwa nje ya uwanja akiuguza maumivu ya misuli aliyoyapata katika mchezo wa ligi dhidi Dodoma Jiji FC uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mfaransa Didier Gomes alisema kuwa kiungo huyo amepona majeraha yake huku akifanya mazoezi chini ya uangalizi wa daktari.

 

Gomes alisema kuwa kiungo ameanza na mazoezi hayo binafsi kwa hofu ya kujitonyesha ili asirejee katika majeraha yake hayo.

 

Sakho amepona majeraha yake ya misuli na hivi sasa yupo chini ya uangalizi wa madaktari wetu ili kuhakikisha anakuwa fiti zaidi.

 

“Hiyo ni baada ya kumuona hayupo fiti, hivyo kwa kuanzia anafanya mazoezi ya fiziki ili kuhakikisha anakuwa fiti zaidi. “inaamini kama akiwa fiti kwa asilimia mia moja, basi Sakho atakuwa msaada mkubwa katika timu,”alisema Gomes.

The post Gomes Aanza Kupambana na Sakho Simba SC appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz