Djuma Arejea Yanga, Apewa Program Maalum-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Djuma Arejea Yanga, Apewa Program Maalum-Michezoni leo

BEKI wa pembeni tegemeo hivi sasa Yanga, Mkongomani Shaban Djuma amejiunga kwenye kambi ya timu hiyo sambamba na kupewa program maalum ya binafsi.

 

Mkongomani huyo hivi karibuni alirejea nchini kwao kwa ajili ya kurekebisha paspoti yake ya kusafiria.

Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja Mkuu wa timu hiyo, Hafidh Saleh alisema kuwa nyota huyo amerejea nchini juzi Jumapili na haraka alijiunga kambini Avic Town, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

 

Saleh alisema kuwa beki huyo mara baada ya kurejea nchini alianza mazoezi ya binafsi ya pekee ili kumuongezea fitinesi ili aendane na kasi ya wenzake.

 

“Djuma tayari amerejea nchini na haraka alianza mazoezi ya binafsi kwa ajili ya kumuongezea fitinesi na program hiyo ni ya siku mbili pekee na anasimamiwa na kocha wa viungo.

“Pia program hiyo ilimhusisha Moloko (Jesus) ambaye yeye alirejea siku moja kabla ya Djuma,” alisema Saleh.

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

The post Djuma Arejea Yanga, Apewa Program Maalum appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz