CHELSEA YAITOA SOUTHAMPTON KWA MATUTA-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

CHELSEA YAITOA SOUTHAMPTON KWA MATUTA-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL Ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako nakutasoma habari zote hata kama hauna MB

WENYEJI, Chelsea wamefanikiwa kutinga Robo Fainali ya Kombe la Ligi England baada ya ushindi wa penalti 5-4 dhidi ya Southampton kufuatia sare ya 1-1 usi wa Jumanne Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.

Kai Havertz alianza kuifungia Chelsea dakika ya 44, kabla ya Che Adams kuisawazishia Southampton dakika ya 47.
Katika mikwaju ya penalti, kipa 
Kepa Arrizabalaga aliokoa penalti ya Theo Walcott wakati Will Smallbone alipiga juu ya lango kuikosesha Southampton penalti mbili, wakati upande wa Chelsea Mason Mount pekee alikosa.
Waliofunga penalti za Chelsea ni Marcos Alonso, Callum Hudson-Odoi, Ben Chilwell na Reece James, wakati  Adam Armstrong, Shane Long na Oriol Romeu ndio waliofunga za Southampton.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz