CAS Yasogeza Mbele Hukumu ya Shauri la Yanga na Morisson-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

CAS Yasogeza Mbele Hukumu ya Shauri la Yanga na Morisson-Michezoni leo

TAREHE ambayo hukumu ya kesi kati ya klabu ya Yanga na mchezaji Bernard Morrison ilikuwa imepangwa, imesogezwa tena mbele mpaka Novemba 23, mwaka huu.

 

Wakili wa Yanga, Alex Mgongolwa akizungumza, ametoa ufafanuzi kuwa hukumu hiyo itatolewa siku yoyote kuanzia sasa mpaka Novemba 23, kwa mujibu wa taarifa waliyopewa na CAS.

 

Mahakama hiyo ya Usuluhishi wa michezo imetoa maamuzi hayo kutokana na upande wa mawakili wa Bernard Morrison kutuma barua ya kielektroniki (E-mail) huko CAS, ambapo walitoa pendekezo kesi hiyo itolewe hukumu kwa kuwa imekua ikiahirishwa mara kwa mara.

 

Awali CAS ilisema itatoa hukumu ya shauri hilo Oktoba 26, lakini haikutoka na itatoka wakati wowote kutoka sasa mpaka Novemba 23.

 

The post CAS Yasogeza Mbele Hukumu ya Shauri la Yanga na Morisson appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz