Bosi Simba Afunguka Kasi ya Yanga-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Bosi Simba Afunguka Kasi ya Yanga-Michezoni leo

MWENYEKITI wa Simba, Murtaza Mangungu, amewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaambia wasiogope kasi ya wapinzani wao Yanga huku akiahidi kuubakisha ubingwa wa Ligi Kuu Bara Msimbazi.

 

Kauli hiyo ameitoa baada ya kuiona Yanga ikiwa kileleni ikiwa na pointi tisa, ikishinda michezo yake
mitatu ya ligi katika msimu
huu.


Simba yenyewe imecheza
michezo miwili kati ya hiyo wametoka suluhu na Biashara United huku ikiwafunga
Dodoma Jiji bao 1-0,
lililofungwa na Mnyarwanda, Meddie Kagere.


“Mechi tatu haziwezi
kuwapa ubingwa au kututoa kwenye mbio za ubingwa. Ligi ni mbio ndefu na sisi Simba ubingwa wetu uko palepale.


“Wanasimba waondoe hofu,
tupo vizuri kama viongozi katika utendaji, pia benchi la ufundi linaloendelea kufanya maandalizi ya kikosi chao,” alisema Mangungu.

The post Bosi Simba Afunguka Kasi ya Yanga appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz