Bocco, Mugalu Wapewa Kazi Maalum Simba SC-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Bocco, Mugalu Wapewa Kazi Maalum Simba SC-Michezoni leo

ZIKIWA zimesalia takribani siku tano kabla ya Simba kuvaana na Jwaneng Galaxy ya Botswana, Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema ana matumaini makubwa na wachezaji wake, John Bocco, Chris Mugalu na Sadio Kanoute kuwa wanaweza kuleta ushindi kutokana na kila siku kuimarika.

 

Oktoba 17, mwaka huu, Simba inatarajia kuwa mgeni wa Jwaneng Galaxy katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya mabingwa Afrika, kabla ya marudiano Oktoba 24, Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Gomes alisema: “Maandalizi yanaendelea vema kama kawaida, naona wachezaji wote wanajituma kila mmoja kwa nafasi yake, nina imani kuwa tutapata ushindi dhidi ya wapinzani wetu.

 

“Imenichukua muda mwingi kukaa na kuangalia wenzetu ni namna gani wanacheza hivyo hii mechi haitakuwa rahisi kwa sababu tunaenda kukutana na timu kubwa na yenye uwezo mkubwa.

 

“Pia tunahitaji kuwa na safu imara ya ulinzi kutokana na mtindo wa uchezaji wa wapinzani wetu, tunahitaji washambuliaji ambao wanaweza kutumia nafasi vizuri kama Bocco, Kanoute na Mugalu kwa sababu hawa ni wachezaji ambao ni rahisi kubadilika kulingana na aina ya mchezo.”

The post Bocco, Mugalu Wapewa Kazi Maalum Simba SC appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz