Beki Yanga SC Ashtukia Jambo-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Beki Yanga SC Ashtukia Jambo-Michezoni leo

BEKI wa kushoto wa Yanga, Yassin Mustafa amefunguka kuwa kwa sasa ushindani wa namba kwenye kikosi chao umeongezeka, hivyo ni lazima apambane ili aingie kwenye kikosi cha kwanza.

 

Yassin amekaa nje ya uwanja kwa nusu msimu baada ya kupata majeraha ambapo msimu huu hajafanikiwa kucheza mchezo wowote kwenye kikosi cha Yanga.

Wakati yeye akiwa nje, kikosi cha Yanga kimeendelea kusheheni wachezaji wa nafasi yake akiwemo Adeyum Saleh, Kibwana Shomari na David Bryson.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Yassin alifunguka kwamba: “Ushindani wa namba kwenye kikosi chetu umekuwa mkubwa, hii ni kutokana na aina ya wachezaji ambao wamesajiliwa msimu huu, hivyo ili upate nafasi ya kuanza kikosini ni lazima upambane.

 

“Kwa upande wangu bado nina nafasi ya kufanya vizuri kikosini, nitapambana mazoezini ili niweze kumshawishi mwalimu pamoja na benchi zima la ufundi.

“Malengo yetu kama timu msimu huu ni kuhakikisha tunatwaa mataji yote makubwa kuanzia Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam, hivyo mashabiki wetu wazidi kutuunga mkono katika kila hatua tunawaahidi furaha msimu huu kwani matarajio yetu ni kukata kiu yao ya kukosa ubingwa kwa muda mrefu.”

ISSA LIPONDA, Dar es Salaam

The post Beki Yanga SC Ashtukia Jambo appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz