Beki Simba Ashonwa Nyuzi Sita, Amwaga Machozi-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Beki Simba Ashonwa Nyuzi Sita, Amwaga Machozi-Michezoni leo

BEKI wa kati wa Simba, Kennedy Juma, ameshonwa nyuzi sita baada ya kupata jeraha kubwa kwenye eneo la jicho kutokana na kuumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji.

 

Kennedy alijikuta anaondolewa na machela kwenye uwanja dakika ya 43 ya mchezo huo kufuatia kupigwa na kiwiko na straika wa Dodoma, Anuar Jabir, ambaye naye alilimwa kadi nyekundu.

 

Mtu wa karibu na daktari wa Simba, Yassin Gembe, aliliambia Championi Jumatatu kuwa hali ya Kennedy inazidi kutengemaa na ameshonwa nyuzi sita jirani na jicho na kwa sasa anaendelea kuimarika.

 

“Kennedy jicho lilivimba kabisa, ile ilikuwa ni rafu mbaya sana ambayo alichezewa na yule mchezaji wa Dodoma, ililazimika ashonwe nyuzi sita ili kuweza kukaa sawa,” alisema mtu huyo.

 

Mtu huyo aliongeza kuwa Kennedy alilia na kusikitika sana baada ya kupata majeraha hayo kwa sababu alijua nafasi yake ya kwenda kambi ya timu ya Taifa imeingia mchanga.

 

“Kennedy alilia na kuumia sana moyoni kwa sababu hiki ndiyo kipindi ambacho alikuwa anaaminiwa timu ya Taifa Stars, sasa maumivu yake.

JOEL THOMAS, Dar es Salaam

The post Beki Simba Ashonwa Nyuzi Sita, Amwaga Machozi appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz