Bao la Simba Lapita Mataifa Matatu-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Bao la Simba Lapita Mataifa Matatu-Michezoni leo

MATAIFA matatu ilibidi yaungane kutengeneza bao la kwanza kwa Simba kwa msimu wa 2021/22, kutokana na kuwa kwenye wakati mgumu katika mechi tatu mfululizo ambazo walicheza.

 

Ikumbukwe kwamba Simba inayonolewa na Kocha Mkuu Didier Gomes ilinyooshwa na watani zao wa jadi Yanga Septemba 25 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii kwa kichapo cha bao 1-0 ikiwa imetoka kunyooshwa pia bao 1-0 dhidi ya TP Mazembe kwenye mchezo wa kirafiki.

 

Ilikuwa kwenye mchezo wa Simba Day, siku ya utambulisho wa wachezaji na benchi la ufundi kwa mashabiki Simba pia ilipoteza Uwanja wa Mkapa.

Kwenye mchezo wa kwanza wa ligi mbele ya Biashara United pia ililazimisha sare ya bila kufungana na kufanya wagawane pointi mojamoja.

 

Iliibuka Uwanja wa Jamhuri, Dodoma baada ya ushindi wa bao 1-0 baada ya mataifa matatu kuungana ili kupata bao hilo na kazi ilianza kwa kipa Aishi Manula yeye ni Mtanzania kisha Chris Mugalu huyu ni raia wa Congo alitoa pasi na mtupiaji alikuwa Meddie Kagere huyu ni raia wa Rwanda.

MARCO MZUMBE, Dar es Salaam

The post Bao la Simba Lapita Mataifa Matatu appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz