Azam FC Waiandalia Dozi Pyramids-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Azam FC Waiandalia Dozi Pyramids-Michezoni leo

KOCHA Msaidizi wa Azam FC, Vivier Bahati, ameelezea mipango yao ya kuwamaliza Pyramids ya nchini Misri.
Azam itacheza mchezo huo wa
raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika wakiwa nyumbani katika viwanja vya Azam Complex Chamanzi nje kidogo ya Jiji la Dar, leo Jumamosi.


Kuelekea mchezo huo wa raundi
ya kwanza Azam imeanza kutesti mitambo kwa kucheza mchezo wa
kirafiki na KMC na kuwafunga 3-2
wikiendi iliyopita.

 

Mabao yote matatu ya Azam yalisababishwa na mshambuliaji wao Ayoub Lyanga huku akitoa asisti kwa Idris Mbombo na Daniel Amoah, na kona ambayo KMC walijifunga.


Akizungumza na Championi
Ijumaa, Bahati amesema kuwa: “Mchezo wetu na KMC ilikuwa kutizama maandalizi tuliyoyafanya kuelekea mchezo wetu na Pyramids
na tunaona vijana wamekaa sawa.”

The post Azam FC Waiandalia Dozi Pyramids appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz