Aliyesajiliwa na Chama Simba, Bado Sana-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Aliyesajiliwa na Chama Simba, Bado Sana-Michezoni leo

INGIZO jipya ndani ya kikosi cha Simba, Jeremia Kisubi bado sana kwa sasa kuanza kikosi cha kwanza kutokana na kutokuwa fiti licha ya uwezo ambao amekuwa akiuonyesha kwenye mazoezi.

 

Nyota huyo aliibuka ndani ya Simba akitokea kikosi cha Tanzania Prisons sababu kubwa inatajwa ni uwezo wake wa kuokoa penalti ambapo aliweza kufanya hivyo katika mchezo wa ligi dhidi ya Simba Uwanja wa Mkapa kwa kuokoa penalti ya Clatous Chama ambaye kwa sasa yupo zake ndani ya kikosi cha RS Berkane.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes alisema kuwa bado kipa huyo anahitaji muda ili aweze kuanza kikosi cha kwanza.

 

“Kisubi alikuwa anaumwa kwa muda wa wiki mbili hivyo bado anahitaji muda zaidi ili kuweza kuanza kikosi cha kwanza lakini hilo halina tatizo atakuwa bora zaidi.

 

“Unajua kwamba Simba tuna makipa wazuri yupo Beno,(Kakolanya) Manula,(Aishi) na Ally, (Salim) hawa wote wanafanya kazi vizuri hivyo Kisubi ni lazima aweze kupata muda ili aweze kuwa bora,” alisema Gomes.

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam

The post Aliyesajiliwa na Chama Simba, Bado Sana appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz