Zahera: Sijaja Kuwa Mkalimani Yanga-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Zahera: Sijaja Kuwa Mkalimani Yanga-Michezoni leo

KOCHA wa zamani wa Yanga ambaye kwa sasa ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Soka la Vijana ndani ya klabu hiyo, Mwinyi Zahera, amefunguka kwamba hajarudi Yanga kwa ajili ya kuwa mkalimani, bali ni kufanya kazi maalum aliyopewa na uongozi.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Zahera alisema: “Watu wanafikiri kuwa pengine nimekuja kufanya kazi ya ukalimani ndani ya Yanga kwa sababu nafahamu kuzungumza Kifaransa na Kiswahili, hapana, mimi nimepewa kazi maalum Yanga kuhakikisha soka la vijana linakua na kuleta faida ndani ya timu.

 

“Yanga ili iweze kupata mafanikio lazima ipitie katika mifumo ya kisasa ikiwa ni pamoja na kuinua soka la vijana, naamini nitafanikiwa ndani ya Yanga kwa kuwa kuna vipaji vingi sana hapa nchini na vitaenda kuinufaisha klabu hii.”

 

Lunyamadzo Mlyuka, Dar es Salaam

 

The post Zahera: Sijaja Kuwa Mkalimani Yanga appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz