Yanga Yawatoa Hofu Mashabiki Mechi ya Simba-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Yanga Yawatoa Hofu Mashabiki Mechi ya Simba-Michezoni leo

YANGA imewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaambia kuwa upo uwezekano mkubwa wa mabeki wake wawili wa kushoto, Yassin Mustapha na David Bryson kuwepo katika Ngao ya Jamii.

Mchezo huo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba unatarajiwa kupigwa Septemba 25, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Wachezaji hao walikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu wakisumbuliwa na majeraha.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo, Frederick Mwakalebela alisema kuwa kikosi kinaendelea vizuri na wachezaji wenye majeraha Bryson na Yassin wameanza mazoezi ya nguvu pamoja na wenzao kwa wiki moja.

Mwakalebela alisema kuwa wachezaji hao wamepona na watakuwa sehemu ya kikosi hicho kitakachoanza katika Ngao ya Jamii.

Aliongeza wachezaji hao hawatakuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza Ligi ya Mabingwa Afrika kutokana na kukosa fitinesi.

“Tunaamini bado tuna kikosi imara cha kufanya vizuri katika msimu huu licha ya kukabiliwa na majeraha kadhaa ya wachezaji. Wachezaji hao ni Bryson na Yassin ambao wanaendelea vizuri. Watakuwepo sehemu ya kikosi kitakachocheza mchezo wa Ngao ya Jamii,” alisema Mwakalebela.

Wilbert Molandi, Dar es Salaam

The post Yanga Yawatoa Hofu Mashabiki Mechi ya Simba appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz