Yanga Yaanza Kunoga Safu ya Ushambuliaji-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Yanga Yaanza Kunoga Safu ya Ushambuliaji-Michezoni leo

UNAWEZA kusema Yanga chini ya Kocha Mkuu, Nassredine Nabi, taratibu inaanza kunoga kutokana na timu hiyo kupata muunganiko mzuri hasa kwenye safu ya ushambuliaji ambayo inaongozwa na Heritier Makambo na Fiston Mayele.


Timu hiyo inayojiandaa na msimu wa 2021/22,
tayari imecheza michezo minne ya kirafiki mpaka sasa ambapo imeshinda mitatu dhidi ya DTB (3-1), Friends Rangers (3-1) na Pan African (1-0), huku ikipoteza mmoja wa kimataifa dhidi ya Zanaco kwa kufungwa mabao 1-2.

 

Kwenye michezo hiyo minne, Yanga wameonesha muunganiko mzuri kwa wachezaji ambao utawasaidia kwenye michuano mbalimbali wakianza na Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali dhidi ya Rivers United ya Nigeria utakaochezwa wikiendi hii.


Msimu uliopita, Yanga ilionekana kuwa na shida
kwenye safu ya ushambuliaji ambapo kwa sasa dawa inaonekana kupatikana kwani safu hiyo kwenye mechi nne ilizochezwa, imefunga mabao matatu.Mayele amefunga mabao mawili kwenye michezo dhidi ya Friends Rangers na Pan African, huku Makambo akifunga bao moja dhidi ya Zanaco.

 

Safu ya ushambuliaji ya Yanga inazidi kunoga kama ambavyo Kocha Nabi amekuwa akipambana iwe na makali ambapo hadi sasa inadhihirisha kwamba, siku akianzishwa mmoja, mwingine akiingia kutokea benchi ataendeleza makali yaleyale.

 

Lakini kama wakianzishwa wote, basi siku hiyo kutakuwa na balaa kubwa na mabeki wa timu pinzani watapata tabu sana wamzuie nane.

 

Yanga kwa sasa inacheza michezo ya kirafiki kwa ajili ya kujiimarisha zaidi katika kujiandaa na msimu ujao.Hivi karibuni, Nabi alinukuliwa akisema: “Kwa sasa natafuta muunganiko wa timu yangu kuanzia kwenye eneo la ulinzi, kiungo na ushambuliaji.

 

“Ukiangalia timu ina wachezaji wengi wapya ambao wanahitaji kuzoeana, hivyo kwa muda huu tunapaswa kuutumia vizuri ingawa naona vijana wameanza kuimarika.” Kuelekea mchezo wa Jumapili dhidi ya Rivers, Makambo amesema:

 

“Mashabiki mje kwa wingi siku ya Jumapili, tuje kuwajaza kwa pamoja, mkumbuke nyinyi ni wachezaji wa 12 uwanjani.”

LEEN ESSAU, DAR

 

The post Yanga Yaanza Kunoga Safu ya Ushambuliaji appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz