Yanga: Tupo Tayari, Simba; Hatuna Presha – Video-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Yanga: Tupo Tayari, Simba; Hatuna Presha – Video-Michezoni leo


SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Simba na Yanga utachezwa kuanzia saa 11:00 jioni ya Jumamosi, 25 Septemba 2021, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Mchezo huo ni maalum kwa ufunguzi wa msimu wa 2021/22.

 

Hayo yamesemwa leo Jumanne, Septemba 21, 2021 na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Mario Ndimbo wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam kuelekea mchezo huo unaowakutanisha mahasimu wawili wa Tanzania.

 

Kwa upande wa Yanga wamesema; “Tunaingia katika mchezo huu dhidi ya Simba tukiwa na kikosi imara, kinaendelea kuimarika siku hadi siku na wale ambao mlikuwa mnawasikia sikia, nao watakuwepo. Sisi tupo imara sana,”- Hassan Bumbuli, Ofisa Habari wa Yanga.

 

Simba nao wamesema; “Simba SC iko tayari. Mara baada ya tamasha la Jumapili, tulipumzika siku mbili na leo timu imeingia kambini na iko salama. Haina majeruhi yoyote. Tumepata mechi za vipimo vya kutosha na hatuna presha kwenye hiyo mechi.” – Ezekiel Kamwaga, Kaimu Ofisa Habari wa Simba.

The post Yanga: Tupo Tayari, Simba; Hatuna Presha – Video appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz