Yanga Kuwakosa Aucho, Mayele, Juma Dhidi ya Rivers Jumapili-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Yanga Kuwakosa Aucho, Mayele, Juma Dhidi ya Rivers Jumapili-Michezoni leo


MSEMAJI wa klabu ya Yanga, Haji Manara leo Septemba 08, 2021 akiongea na wanahabari Makao yao Makuu ya klabu hiyo Jangwani jijini Dar es Salaam amesema watawakosa wachezaji wao watatu Khalid Aucho, Fiston Mayele na Juma Shabani kwenye mchezo dhidi ya Rivers United ya Nigeria siku ya Jumapili Septemba 8, 2021 kwenye Uwaja wa Mkapa kutokana na ITC zao kuchelewa.

 

“Tutawakosa wachezaji wetu Khalid Aucho, Fiston Mayele na Juma Shabani kuelekea mchezo wetu dhidi ya Rivers United kutokana na ITC zao kuchelewa, kiukweli ni pengo hatuwezi kusema sio pengo ila ondoeni hofu tumesajili wachezaji bora wengi”

“Mpaka sasa hatujapata idadi ya mashabiki watakaoruhusiwa kuingia uwanjani, tunasubiri taarifa ya CAF kupitia TFF ndani ya saa 24 tunaweza kuipata ndio maana hatujatangaza viingilio kwanza”

“Kesho nitakutana na vikundi vya hamasa. Hatuendi uwanjani kukaa, tunatakiwa kuanikiza na kuwapa nguvu wachezaji muda wote. Nilikuwa naona wivu sana wenzangu mlikuwa mnatumia nguvu kidogo tu uwanja unajaa, mimi ilibidi nitumie nguvu nyingi sana”
“Malengo yetu sio kufika tu ‘Group Stage’ ni kuvuka na kufika mbali zaidi. Sisi ndio mabingwa na ndio timu ya kwanza Tanzania kufika Group Stage na Quarter Final kwenye Ligi ya Mabingwa na Slogan tunayokwenda nayo ni The Return Of Champions” amesema Haji Manara.

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

The post Yanga Kuwakosa Aucho, Mayele, Juma Dhidi ya Rivers Jumapili appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz