Yanga Kukiwasha na Rivers United Kwa Mkapa Leo-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Yanga Kukiwasha na Rivers United Kwa Mkapa Leo-Michezoni leo

LEO Jumapili Yanga, itakuwa na kazi moja tu, nayo ni kuhakikisha inaibuka na ushindi wa maana katika mchezo wa kwanza wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United ya Nigeria utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar.


Mara baada ya mchezo
wa leo, Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wa marudiano na timu hiyo, Septemba 19, mwaka huu nchini Nigeria.

 

Sasa kuelekea mchezo wa leo, wachezaji wa Yanga wametamba kuwa, kazi wataimalizia Uwanja wa Mkapa, ili wakienda Nigeria, iwe rahisi kwao kutinga hatua inayofuata huku malengo makubwa ni kufika hadi hatua ya makundi.

 

Yanga itawakosa wachezaji wake watatu wapya ambao ni Djuma Shabani, Fiston Mayele na Khalid Aucho ambao vibali vyao vimekuwa na shida, hivyo hawaruhusiwi kucheza.

 

Licha ya Yanga kuwakosa nyota hao, lakini bado uongozi wa klabu hiyo umetamba kuwa wana kikosi bora na kipana ambacho kinatosha kuwapa ushindi.Kuelekea mchezo huo, Msemaji wa Yanga, Haji Manara ambaye amekuja na msemo wa hamasa kuwa ‘Mabingwa Tumerejea’, alisema licha ya kuwakosa Aucho, Djuma na Fiston, lakini wana imani na kikosi chao kwani kinaweza kupata matokeo katika mchezo huo.

 

“Tuna imani licha ya kuwakosa wachezaji hao watatu ambao ni muhimu lakini bado wachezaji ambao watasalia wataweza kuipa ushindi Yanga katika mchezo wetu, hivyo Wanayanga msiwe na presha kwani kila kitu kitakuwa sawa,” alisema Manara.

 

Naye Kiungo wa Yanga, Feisal Salum, alisema:
“Malengo yetu ni kufika
mbali, tunahitaji ushindi na tumejipanga kuhakikisha tunapamabania hilo ili tuwe ndani ya malengo yetu.”


KIKOSI
KITAKAVYOKUWA
Kocha Mkuu wa Yanga,
Nasreddine Nabi, leo Jumapili baada ya kuwakosa mastaa wake hao watatu, huenda upande wa beki wa kulia pengo la Djuma likazibwa na Kibwana Shomari ambaye ndiye aliyecheza vizuri msimu uliopita.Kwa upande wa Aucho, huenda nafasi yake ikachukuliwa na Zawadi Mauya ambaye katika mchezo dhidi ya Zanaco alicheza katika eneo la kiungo mkabaji.

 

Yanick Bangala Litombo ambaye ni kiraka cha kazi, huenda akapangwa katika eneo la beki wa kushoto kutokana na nafasi hiyo kupwaya kitendo ambacho kilimlazimu kocha Nabi kumtumia Kibwana Shomari ambaye atarudi rasmi katika nafasi yake ya beki wa kulia.

 

Kwa upande wa ushambuliaji, kukosekana kwa Fiston Mayele, watapangwa Heritier Makambo sambamba na Yacouba Songne.Kikosi kamili kitakuwa hivi; Diarra Djigui, Kibwana Shomari, Yannick Bangala Litombo, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Mukoko Tonombe, Feisal Salum, Jesus Moloko, Yacouba Songne na Heritier Makambo.

KAULI YA NABI
Akizungumza na Spoti
Xtra, Kocha Nabi alisema: “Tunatarajia mchezo mgumu dhidi ya Rivers, lakini tumejiandaa kuhakikisha tunapata matokeo mazuri katika uwanja wetu wa nyumbani ili kufikia malengo yetu ya kufika mbali katika michuano hii.

 

“Ukiachana na malengo ya klabu kwa ujumla, lakini binafsi ninahitaji kuona klabu hii ikifika angalau hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa na si chini ya hapo.

MARCO MZUMBE NA JOEL THOMAS, Dar es Salaam

The post Yanga Kukiwasha na Rivers United Kwa Mkapa Leo appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz