Viatu vya Onyango Mikononi mwa Kennedy-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Viatu vya Onyango Mikononi mwa Kennedy-Michezoni leo

MZAWA Keneddy Juma, mwili jumba beki wa mpira taratibu anaanza kuwa fiti kila anapotokea benchi kwenye mechi za ushindani ndani ya Simba licha ya kutoaminika mara kwa mara mbele ya Didier Gomes ambaye ni Kocha Mkuu.

 

Ikumbukwe kwamba Kennedy ni mshikaji asiyependa kuzungumza kwa maneno ila matendo na kila anapopata mpira rekodi zinaonyesha sio mtu wa mambo mengi na pasi anazopenda kuzitoa ni zile pasi fupifupi na ndefu huwa anamuachia Pascal Wawa.

 

Kwenye mechi mbili za Gomes, Kennedy akitokea benchi aliweza kuonyesha kile alichonacho kwa kutimiza majukumu yake vizuri, ilikuwa ni ile ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Kaizer Chiefs Mei 22, wakati Simba ikishinda mabao 3-0.

Beki huyo alitokea benchi na aliyeyusha dakika 56, baada ya Onyango kuumia na aliweza kufanya hivyo kwa kuzuia mashambulizi ya mshambuliaji msumbufu na wa bei ghali Samir Nurkovic. Aliweza kufanya hivyo juzi Septemba 25, alipoingia kuchukua nafasi ya Onyango.

 

Aliweza kuvaa viatu vizuri vya Onyango kwa kuwa aliweza kutuliza mashambulizi na kutibua mipango ya Fiston Mayele, Heritier Makambo waliokuwa kwenye kasi yao wakati Simba ikipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na kupoteza taji la Ngao ya Jamii.

 

Kwenye ligi msimu wa 2020/21, kwenye mechi 34 ni mechi 16 aliweza kucheza na alikosekana katika jumla ya mechi 18.

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam

The post Viatu vya Onyango Mikononi mwa Kennedy appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz