TP Mazembe Walivyozuiwa Getini-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

TP Mazembe Walivyozuiwa Getini-Michezoni leo

MASHABIKI wa Klabu ya TP Mazembe ya DR Congo jana walionja joto ya jiwe baada ya kuzuiwa getini walipokuwa kwenye harakati za kuingia uwanjani kushudia timu yao.

 

Ilikuwa ni jana kwenye tamasha la Simba Day Uwanja wa Mkapa mapema mashabiki hao walijitokeza kwa wingi ili kuweza kuingia ndani ya uwanja.

 

Ilikuwa ngumu kwao kuingia uwanjani kwa sababu hawakuwa na vibali vya kuingia uwanjani pamoja na tiketi ambazo zingewapa nafasi ya kuingia kuutazama mchezo huo.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu moja ya mashabiki wa TP Mazembe ameeleza kuwa walikuwa na ruhusa kutoka kwenye timu yao hivyo walipaswa kuingia uwanjani bila vikwazo vyovyote japokuwa hawana tiketi ila walishapata ruhusa kutoka kwenye menejimenti ya timu.

 

Aidha, mmoja ya walinzi wa siku hiyo alilieleza Championi Jumatatu kuwa wamezuiwa kuingia uwanjani kwa sababu uwanja ulikuwa umejaa na hakuna sehemu ya wao kukaa wala kusimama.

SALUMU SADIKI, Dar es Salaam

The post TP Mazembe Walivyozuiwa Getini appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz