Taifa Stars Mguu Sawa Kuivaa Madagascar-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Taifa Stars Mguu Sawa Kuivaa Madagascar-Michezoni leo

BAADA ya kumalizana na DR Congo kwenye mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia uliochezwa Uwanja wa TP Mazembe, Septemba 2 na ngoma kukamilika kwa kufungana bao 1-1 mchezo unaofuata ni leo Septemba 7.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa majira ya saaa 10:00, huku imani kubwa kwa Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ikiwa ni kupata ushindi.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo alisema kuwa maandalizi yapo vizuri na Watanzania waendelee kuwa bega kwa bega na timu yao.

“Mchezo ujao kwa timu ya taifa ya Tanzania ni dhidi ya Madagascar baada ya kumalizana na DR Congo, maandalizi yanakwenda vizuri hivyo ni mashabiki waendelee kuiunga mkono timu yao,” alisema.

Tayari maandalizi kuelekea kwenye mchezo huo yanaendelea ambapo Poulsen alisema kuwa wanahitaji ushindi kwenye mchezo huo ili waweze kutimiza lengo la kufuzu Kombe la Dunia, 2022, Qatar.

 

LUNYAMADZO MLYUKA ,

Dar es Salaam

The post Taifa Stars Mguu Sawa Kuivaa Madagascar appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz