Straika Mkongo: Nitafunga Sana-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Straika Mkongo: Nitafunga Sana-Michezoni leo

BAADA ya kuanza vizuri maisha yake mapya ndani ya kikosi cha Azam kwa kufunga bao moja katika ushindi wa mabao 3-1 walioupata katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Horseed ya Somalia, Straika Mkon­gomani, Idris Mbombo amefunguka kuwa atafun­ga mabao mengi zaidi msimu ujao.

 

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika uliopigwa juzi Jumamosi, Mbombo aliifungia Azam bao la pili dakika ya 73 ya mchezo huo ambao Azam walishinda kwa mabao 3-1.

 

Mbombo alikamili­sha usajili wake ndani ya Azam na kutambulishwa rasmi Julai 31, mwaka huu akitokea kwenye kikosi cha klabu ya El Gouna in­ayoshiriki Ligi Kuu nchini Misri ambapo alisaini mkataba wa miaka miwili.

 

Akizungumza na Cham­pioni Jumatatu, Mbombo alisema: “Kwangu kama mchezaji ni jambo la kushukuru Mungu ku­weza kufunga bao ambalo limeisaidia timu yangu kupata ushindi muhimu siku ya Jumamosi dhidi ya Horseed ya Somalia.

 

“Licha ya kufunga bao hilo lakini binafsi naona bado nina kazi kubwa ya kufanya, ili kurejea katika kiwango changu, hii ni kwa sababu kwa muda mrefu nilikuwa benchi kule El Gouna, hivyo nitapambana mazoezini ili kufunga mabao mengi zaidi kwa kila nafasi nita­kayoaminiwa na kocha.”

 

JOEL THOMAS, DAR ES SALAAM

The post Straika Mkongo: Nitafunga Sana appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz