Solskjaer Amtabiria Makubwa Sancho-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Solskjaer Amtabiria Makubwa Sancho-Michezoni leo

 

 

KOCHA wa Man United, Ole Gunnar Solskjaer amesema anaamini kuwa winga wake Jadon Sancho atakuwa mshambuliaji mahiri wa Man United miaka kadhaa ijayo.

Sancho alijiunga na United akitokea Borrusia Dortmund na ameshindwa kuonyesha makali yake kabla ya mchezo wa jana dhidi ya West Ham.

Hata hivyo, mashabiki wa Man United wanaamini kuwa anatakiwa kupewa muda na huko mbele atafanya vizuri.

Kocha huyo wa United amesema anaamini kuhusu uwezo wa kinda huyo na hana shaka kuwa anaweza kuwa staa wa United miaka mingi ijayo.

Amesema kwa sasa anamuona akiendelea kujifunza jinsi ya kuitumikia United lakini pia jinsi ya kucheza Ligi Kuu ya England, sehemu ambayo ni ngumu sana kwa mchezaji yoyote kucheza.

“Namuona miaka ijayo akiwa staa mkubwa sana hapa United, sina shaka hata kidogo na uwezo wake uwanjani.

Jinsi alivyoanza haliwezi kuwa tatizo kwangu kwa kuwa naamini kuhusu uwezo wake wa siku zote.

“Kama ambavyo nimekuwa nikisema amekuwa akifanya mazoezi vizuri na kujifunza tabia za Ligi Kuu England, anatakiwa kupewa moyo kwa sasa lakini baadaye ataamka na kuwa bora kwa kuwa anafahamu mashindano makubwa yakiwemo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya aliyocheza akiwa na Dortmund,” alisema kocha huyo.

United walifanikiwa kumsajili mchezaji huyo raia wa England kwa kitita cha pauni milioni 73, kutoka kwenye kikosi cha Borussia Dortmund.

 

MANCHESTER, England

 

The post Solskjaer Amtabiria Makubwa Sancho appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz