Simba Day: Simba Kukipiga na TP Mazembe kwa Mkapa-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Simba Day: Simba Kukipiga na TP Mazembe kwa Mkapa-Michezoni leo

 

KATIKA kuadhimisha kilele cha Tamasha la Simba Day mwaka huu Klabu ya Simba inatarajiwa kucheza mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Mabingwa mara tano (5) wa Ligi ya Mabingwa Afrika TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

 

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba SC, Barbara Gonzalez amethibitisha kuwa Klabu ya TP Mazembe ya DR Congo ndiyo wageni waalikwa wa Simba katika mchezo wa Simba Day 2021.

 

“Nina furaha kuwatangazia Wanasimba na Watanzania wote kwa ujumla kuwa tutacheza na TP Mazembe siku ya Simba Day September 19 mwaka huu 2021. Tayari tumekamilisha taratibu zote za kuwaalika na sasa ni rasmi kuwa wao ndiyo watakuwa wageni wetu”, amesema Barbara.

 

 

Barbara ameongeza kuwa TP Mazembe ni mojawapo ya timu zenye heshima kubwa Barani Afrika na ni heshima kubwa kwa Simba kupata fursa ya kucheza nayo.

 

Barbara pia amesema kuwa lilikuwa lengo la uongozi na benchi la ufundi kuhakikisha Simba inapata timu nzuri Ili kujua ni wapi hasa kikosi cha msimu huu kipo kwenye maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Bara Kuu na Ligi ya Mabingwa Afrika.

TP ndio Mabingwa wa Ligi Kuu nchini DR Congo msimu uliopita wa 2020/2021 ni Mabingwa mara 5 wa CAF Champion League, ni Mabingwa mara 2 wa CAF Confederation Cup, ni Mabingwa mara 1 wa kombe la washindi Afrika na Mabingwa mara 3 wa Super Cup Afrika.

 

Tamasha hilo la Simba Day linatarajiwa kufanyika September 19, 2021 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

The post Simba Day: Simba Kukipiga na TP Mazembe kwa Mkapa appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz