Samuel Eto’o Atangaza Kugombea Urais-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Samuel Eto’o Atangaza Kugombea Urais-Michezoni leo

NYOTA wa soka nchini Cameroon, Samuel Eto’o ametangaza kugombea Urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Cameroon. Eto’o ametoa tangazo hilo jana  Jumanne kupitia ukurasa wake rasmi wa Facebook.

 

“Nimeamua kuchukua uamuzi huu kwasababu ya kuipenda Cameroon na kupenda soka yetu…. ni wakati wa kujenga upya mpira wetu,” alielezea Eto’o katika taarifa yake hiyo.

 

Eto’o anaweza kukupambana na kizuizi kwa kile kinachodaiwa kuwa ana uraia pacha wa Hispania tangu wakati akicheza Barcelona.

 

Miongoni mwa masharti yanayotakiwa kuwa mgombea wa urais wa shirikisho la mpira wa miguu la Cameroon, ni marufuku ya kuwa na utaifa wa kigeni.

 

Samuel Eto’o ni kigogo wa tatu wa zamani kugombea urais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Cameroon. Hata hivyo, bado haijulikani ikiwa ugombea wake utathibitishwa. Uchaguzi umepangwa kufanyika Desemba 11.

The post Samuel Eto’o Atangaza Kugombea Urais appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz