Sakho, Banda Wampa Kiburi Bocco-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Sakho, Banda Wampa Kiburi Bocco-Michezoni leo

SIMBA imeanza jeuri katika kuelekea msimu ujao, ni baada ya kutamba hawataacha kikombe chochote cha ubingwa watakachopambania pamoja na watani wao wa jadi, Yanga.

Hiyo ni kutokana na usajili bora na wakisasa ambao Simba imeufanya katika kuelekea msimu ujao ambao timu hiyo imepanga kubeba Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kati ya usajili bora wanaoutambia Simba ni wa Peter Banda, Ousmane Sakho, Duncan Nyoni, Sadio Kanoute, Inonga Baka ‘Varane’, Jeremiah Kisubi, Denis Kibu na Yusuf Mhilu.

Akizungumza na Championi Jumatatu, nahodha na mshambuliaji wa timu hiyo, John Bocco alisema maandalizi ya kambi yao waliyoyafanya Karatu, Arusha yamewapa hali ya kujiamini ikiwemo kubeba kila kikombe wanachokiwania.

Bocco alisema kuwa amefurahishwa na ubora, viwango vya wachezaji wapya waliowasajili kwa kuanzia mazoezini na katika michezo ya kirafiki ambayo wamecheza.

Aliongeza kuwa ana matumaini makubwa ya kubeba kila taji la ubingwa ikiwemo ligi na Kombe la FA na lile la Kombe la Mapinduzi ambalo katika msimu uliopita lilichukuliwa na Yanga.

“Katika msimu uliopita kwa makombe ya hapa nchini, lile la Mapinduzi pekee ndiyo ambalo hatujalichukua lakini mengine yote ya ligi na FA tulichukua sisi.

“Hivyo hatutaki masihara tunataka kuona tunabeba kila kombe tutakalolishindania katika msimu huu na hiyo ni kutoka na ubora wa kikosi chetu tulichokisajili,”alisema Bocco.

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

The post Sakho, Banda Wampa Kiburi Bocco appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz