Ronaldo Avamiwa Na Mashabiki Akitoka Tizi-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Ronaldo Avamiwa Na Mashabiki Akitoka Tizi-Michezoni leo

CRISTIANO Ronaldo juzi alionekana kwenye mazoezi ya timu yake ya Man United kwa mara ya kwanza huku akivamiwa na mashabiki waliolizingira gari lake la kifahari aina ya Lamborghini 4/4 wakati akitoka mazoezini, waliomshangilia na wengine wakinyanyua mabango ya kuonyesha kufurahishwa na ujio wake klabuni hapo.

Ronaldo, 36, ambaye alikuwa na gari lake aina Lamborghini 4/4 yenye thamani ya pauni 160,000, alionekana akiwa makini sana wakati anatoka na kuingia kwenye mazoezi hayo.

 

Mashabiki ambao walikuwa nje ya geti hilo walisikika wakimwambia tunafurahi kukuona tena umerudi hapa.

 

Hata hivyo, sasa mashabiki wa United wajiandae kuona magari makali aina ya Ferrari Monza, Rolls Royce, Mercedes G-Wagon na Bugattis ambayo yanamilikiwa na Ronaldo yakiingia mazoezini hapo.

The post Ronaldo Avamiwa Na Mashabiki Akitoka Tizi appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz