Nabi Afunguka Majukumu ya Kaze Yanga-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Nabi Afunguka Majukumu ya Kaze Yanga-Michezoni leo

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amesema moja ya kitu ambacho anashukuru ni urejeo wa Cedric Kaze kwenye timu hiyo kwa kuwa amekuja kufanya kazi yake iwe nyepesi.

 

Nabi aliyataja majukumu ya Kaze kwenye timu hiyo kuwa ni kumsaidia kuwasilisha programu kwa wachezaji kwa kuwa yeye ni mjuzi wa mambo na faida kubwa aliyonayo ni uwezo wa kuzungumza lugha zote ambazo wachezaji wa Yanga wanazungumza ambazo ni Kingereza, Kifaransa na Kiswahili.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Nabi alisema kabla ya ujio wa Kaze kwa kipindi ambacho alikuwa anafanya kazi peke yake alikuwa anapitia wakati mgumu kwa sababu alikuwa anafanya kazi nyingi kwa wakati mmoja jambo ambalo lilifanya awe anachoka sana.

 

“Najikuta mwenye bahati sana msimu huu kutokana na urejeo wa Kaze kwenye timu, Kaze ni mjuzi wa kazi zetu na aliwahi kupita hapa na anaifahamu timu na wachezaji vizuri sana.

 

“Atakuwa msaada mkubwa sana kwenye timu yetu kwa sababu anajua kuzungumza lugha zote ambazo wachezaji wa Yanga wanazungumza jambo ambalo awali lilikuwa linanipa ugumu na kupelekea kufanya kazi kubwa kila siku,” alisema Nabi.

 

Katika hatua nyingine, Nabi ameomba siku 30 kwa ajili ya kuimarisha zaidi kikosi chake kiwe na makali zaidi kwa msimu huu.

 

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, alisema: “Tunaenda kucheza mchezo wetu wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar, Wanayanga tunapaswa kushikamana vizuri zaidi ya hapo mwanzo.

 

“Hatukuwa na muda wa kujiandaa zaidi kama wenzetu ila kwa sasa Kocha Nabi ameomba siku 30 zaidi za kuiandaa timu bora zaidi ya ile iliyocheza na Simba.

 

“Malengo yetu sio tu kumzuia Simba kuchukua ubingwa, bali tunataka kumzidi kwa pointi ili tuchukue ubingwa wa ligi kuu kwa msimu ujao.”

ISSA LIPONDA NA LEEN ESSAU, DAR

The post Nabi Afunguka Majukumu ya Kaze Yanga appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz