Mwamuzi Simba vs Yanga pasua kichwa-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mwamuzi Simba vs Yanga pasua kichwa-Michezoni leo

ZIKIWA zimebaki siku nne kwa sasa mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Simba dhidi ya Yanga uchezwe Uwanja wa Mkapa, Dar, habari zinaeleza kuwa bado mwamuzi wa mchezo huo ni pasua kichwa.

 

Habari kutoka chanzo cha kuaminika, zimeliambia Spoti Xtra kuwa mpaka sasa haijajulikana siku ya kufanya kikao kwa ajili ya kujadili waamuzi ambao watachezesha mchezo huo.

 

“Mchezo upo ila mpaka sasa bado haijaamuliwa ni nani atakuwa mwamuzi wa mchezo huo, pia haijafahamika siku ya kukutana kujadili kuhusu mwamuzi kwani mambo bado,” kilisema chanzo hicho.

 

Ikumbukwe kuwa, Agosti 30, 2020 katika mchezo wa Ngao ya Jamii uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, mwamuzi wa kati alikuwa ni Ramadhan Kayoko, alishirikiana na Mohamed Mkono, Ahmed Arajiga, Ramadhani Mwinyimkuu na Abubakari Mturo kuamua mchezo huo.

 

Hivi karibuni, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Cliford Ndimbo, aliliambia Spoti Xtra kuwa, maandalizi yanakwenda vizuri kuelekea mchezo huo.

Lunyamadzo Mlyuka, Dar es Salaam

The post Mwamuzi Simba vs Yanga pasua kichwa appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz