Morrison Alia Kuwakosa Yanga-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Morrison Alia Kuwakosa Yanga-Michezoni leo

KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison, amejikuta akitoa kilio kufuatia kutokuwa sehemu ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga, inayotarajiwa kuchezwa Septemba 25, mwaka huu katika Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Morrison hatakuwa sehemu ya mchezo huo, kufuatia kuwa na adhabu ya kutocheza mechi tatu, baada ya kuvua bukta wakati akishangilia ushindi wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Morrison alisema: “Watu wengi wamesahau kama mimi sitakuwa sehemu ya mchezo huo wa Ngao ya Jamii, kutokana na kutumikia adhabu ila kungekuwa na uwezo wa kuomba adhabu isogezwe mbele ningeomba ili niwalambishe juisi Yanga, jambo ambalo halitawezekana tena japo tutashinda.”

MUSA MATEJA, Dar es Salaam

The post Morrison Alia Kuwakosa Yanga appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz