Molinga Atamba Kuwamaliza Yanga-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Molinga Atamba Kuwamaliza Yanga-Michezoni leo

MSHAMBULIAJI mpya wa Namungo, David Molinga ‘Falcao’ ametamba kuwa amejipanga kufanya vizuri katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara hususani atakapokutana na waajiri wake wa zamani klabu ya Yanga.

 

Molinga alikamilisha usajili wake wa kujiunga na Namungo na kutangazwa rasmi Septema 1, mwaka huu akitokea kwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Zambia klabu ya Zesco United, aliyoichezea msimu uliopita.

 

Mkongomani huyo amewahi kuichezea Yanga kwa msimu wa 2019/20, ambapo alimaliza msimu huo akiwa mfungaji bora wa Yanga kufuatia kutupia kambani mabao 12.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Molinga alisema: “Ni jambo zuri kwangu kurejea tena na kucheza soka Tanzania, kwangu nchi hii ni kama nyumbani kwangu na nimefarijika sana kujiunga na Namungo. Deni kubwa ambalo ninalo ni kuhakikisha naonyesha uwezo mkubwa na kuwathibitishia viongozi wa Namungo kuwa hawakukosea kuniamini.

 

“Natarajia msimu ujao utakuwa mgumu kutokana na maandalizi ya kila timu ikiwemo suala la usajili, lakini kama mchezaji nimejipanga kuhakikisha nafanya vizuri kwenye kila mchezo hususani pale nitakapokutana dhidi ya waajiri wangu wa zamani Yanga,” alisema mchezaji huyo mwenye mwili nyumba.

MUSA MATEJA NA JOEL THOMAS

The post Molinga Atamba Kuwamaliza Yanga appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz