Mo Awapa Mtihani Mzito Mastaa Simba-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mo Awapa Mtihani Mzito Mastaa Simba-Michezoni leo

KUELEKEA mchezo wa leo dhidi ya Yanga, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ amewapa mtihani mzito mastaa wa kikosi hicho kwa kuwataka kuhakikisha wanapigana kufa na kupona na kuonyesha thamani ya jezi ya Simba kwa kuibuka na ushindi katika mchezo huo.

 

Mo aliibuka kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika juzi Alhamisi katika Viwanja vya Mo Arena, Bunju ikiwa ni siku chache kabla ya mechi hiyo ya Ngao ya Jamii.

 

Leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, Simba watakuwa wenyeji wa Yanga katika mchezo wa Ngao ya Jamii, unaotarajiwa kupigwa majira ya saa 11:00 jioni.

 

Chanzo chetu cha kuaminika kutoka ndani ya Simba kimelitonya Championi Jumamosi, kuwa bosi huyo amewataka wachezaji kuhakikisha wanapambana kufa na kupona na kuonyesha thamani ya jezi ya Simba kwa kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mchezo huo.

 

“Katika kikao cha Mwenyekiti wetu wa Bodi ya Wakurugenzi, Mohammed Dewji ‘Mo’ na wachezaji alijaribu kuwagusia mambo mengi hasa kutokana na umuhimu wa mchezo wetu wa kesho (leo) dhidi ya Yanga.

 

“Lakini kubwa zaidi ni kuwaasa wachezaji kupambana kufa na kupona kuhakikisha wanaonyesha thamani ya jezi ya Simba kwa kuibuka na ushindi, na kuhusu ahadi hilo ni suala ambalo amelifanya kuwa siri,” kilisema chanzo hicho.

 

Kwa upande wake beki wa Simba, Erasto Nyoni alisema: “Ni kweli bosi wetu alikuja kututembelea mazoezini na lengo kuwa lilikuwa ni kutupa hamasa zaidi na kutusisitiza kuhusu umuhimu wa kushinda hii mechi ya (kesho) leo, pia ameahidi kutupa ushirikiano mkubwa ili tuweze kufikia malengo yetu sisi kama timu ambayo ni kutwaa ubingwa wa Ngao ya jamii na Ligi kwa ujumla.

 

“Kwa upande wetu sisi kama wachezaji tumejipanga vizuri kabisa kuhakikisha tunafikia malengo ya timu

JOEL THOMAS NA HAWA ABOUBAKHARI, Dar

The post Mo Awapa Mtihani Mzito Mastaa Simba appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz