Mo Aimaliza Yanga SC Mapema tu-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mo Aimaliza Yanga SC Mapema tu-Michezoni leo

BAADA ya kikao kizito kilichofanyika kati ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’, Mtendaji wa Klabu, Barbara Gonzalez na Kocha Mkuu, Didier Gomes, imebainika kwamba wachezaji wameahidiwa bonasi mara tatu zaidi ya waliyowahi kupewa endapo wataifunga Yanga, leo Jumamosi katika mchezo wa Ngao ya Jamii.

 

Kikao hicho kilifanyika fasta baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya TP Mazembe, kwenye Simba Day, ambapo Mo alitaka kukutana na Gomes kuweka mikakati ya kuimaliza Yanga.

 

Chanzo chetu kutoka ndani ya Simba, kimeliambia Spoti Xtra kuwa: “Mo kwenye kikao alichofanya wakiwa na CEO Barbara, amemtuma Kocha Gomes awaambie wachezaji wake kuwa endapo watashinda mchezo huo atawapa bonasi ya mara tatu zaidi ya ile ambayo amekuwa akiwaahidi kwenye mchezo dhidi ya Yanga kila mwaka.

 

“Unajua Mo kabla ya Simba Day, hakuwepo nchini, aliporejea siku husika alitarajia kupata furaha kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe, ikashindikana kutokana na kufungwa bao 1-0, hivyo anaitaka furaha hiyo dhidi ya Yanga ndio sababu ya kuwaita Barbara na Gomes kwa ajili ya kuwahamasisha zaidi wachezaji.

 

“Baada ya kikao alimwambia Gomes akawaambie wachezaji kambini kuwa wanapaswa kushinda mchezo huo kwani kuna bonasi kubwa zaidi, unajua mchezo huo utakuwa wa ufunguzi wa msimu, hivyo endapo wachezaji watafanya vizuri itawaongezea hamasa zaidi hata kwenye michezo inayofuata ya ligi na ule wa Ligi ya Mabingwa Afrika.”

 

Spoti Xtra lilimtafuta Kaimu Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, ambapo alisema: “Watu wanatakiwa watambue ukubwa wa Simba, kwa sasa sio timu tena ya kujikusanya wajumbe wa kamati mbalimbali kambini kama nia ya kutoa hamasa kama huko nyuma.”

MUSA MATEJA, Dar es Salaam

The post Mo Aimaliza Yanga SC Mapema tu appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz