Mayele Achambua Ufundi wa Bao Lake-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mayele Achambua Ufundi wa Bao Lake-Michezoni leo

BAADA ya kufunga bao ambalo liliipa ushindi Yanga dhidi ya Simba katika mchezo wa Ngao ya Jamii, mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele amelichambua bao lake ambalo alimfunga kipa wa Simba, Aishi Manula katika mchezo uliofanyika  Uwanja wa Mkapa Jumamosi, Septemba 25.

 

Mayele mwenye uraia wa DR Congo amejiunga na Yanga katika dirisha kubwa mwaka huu mpaka sasa amefanikiwa kuifungia Yanga mabao 5 katika michezo 6 aliyoichezea timu hiyo ikiwemo na ile ya kirafiki ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu 2021/22 ulioanza jana Jumatatu.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mayele alisema kuwa anafuraha kubwa kuweza kuifungia Yanga bao muhimu katika mechi muhimu kwani ilikuwa ndoto yake kuhakikisha anaifunga Simba baada ya kusajiliwa na Yanga huku akilichambua bao lake kwa kusema kuwa ilibidi aunganishe ile pasi ya Farid Musa ili kipa Aishi Manula ashindwe kujipanga kwani kama angetuliza basi anaamini ilikuwa rahisi kwa Manula kuweza kuudaka mpira ule.

 

“Nafurahi kuona nimefanikiwa kuifunga Simba baada ya kusajiliwa ndani ya Yanga nilitambua moja ya jukumu kubwa kwangu ni kuwapa raha mashabiki wa Yanga kwa kuhakikisha kuwa naifunga Simba, niliahidi nitawafunga na nashukuru Mungu nimefanikiwa katika hilo.

 

“Kabla sijaupiga ule mpira niliopewa na Musa tayari nilimuona Kipa wa Simba, Aishi Manula akiwa amesogea mbele kupunguza goli hivyo akili ya haraka ilinituma niuunganishe na nisiutulize kwani ningempa kipa nafasi ya kujipanga na mabeki kunizonga hivyo nikaunganisha moja kwa moja nikafanikiwa kufunga nashukuru katika hilo,” alisema Mayele.

MARCO MZUMBE, Dar es Salaam

The post Mayele Achambua Ufundi wa Bao Lake appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz