Mauya Apewa Kazi Maalum kwa Kanoute-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mauya Apewa Kazi Maalum kwa Kanoute-Michezoni leo

KIUNGO mkabaji wa Yanga, Zawadi Mauya amesogezwa mbele kucheza namba nane katika mchezo wa Ngao ya Jamii kwa lengo la kupunguza makali ya kiungo mpya wa Simba raia wa Mali, Sadio Kanoute.

 

Hiyo ni katika kuhakikisha timu hiyo inapata ushindi katika mchezo huo unatarajiwa kupigwa leo kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

 

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya benchi la Ufundi la Yanga, upo uwezekano mkubwa wa Mauya kucheza  namba na nane huku Aucho akipangwa sita.

 

Chanzo hicho kilisema kuwa katika mazoezi ya timu hiyo kocha mkuu wa timu hiyo, Nassredine Nabi ameonekana akimuandaa Mauya kucheza nafasi hiyo ambayo atakuwa akikutana mara kwa mara uwanjani na Kanoute.

 

Kiliongeza kuwa Mauya atacheza nafasi hiyo baada ya kukosekana Mkongomani, Mukoko Tonombe ambaye alikuwa akiicheza katika michezo iliyopita.

 

“Nabi tayari amekamilisha maandalizi yake katika kuelekea dabi hiyo, timu bado haijaungana vizuri lakini tayari ametengeneza kikosi cha ushindi.

 

“Katika mchezo huo wapo wachezaji watakalolikosa pambano akiwemo Mukoko ambaye tayari amepatikana mbadala wake naye ni Mauya atakayecheza namba nane na Aucho sita.

 

“Kazi yake kuwa Mauya ni kuzuia mashambulizi kwa kuanzia juu kwa lengo la kutowapa nafasi viungo wa Simba kupeleka mashambulizi golini kwetu,” kilisema chanzo hicho.

 

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema kuwa: “Maandalizi yamekamilika kwa kiwango kikubwa, wachezaji wana morali katika kuhakikisha tunapata ushindi,” alisema Bumbuli.

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

The post Mauya Apewa Kazi Maalum kwa Kanoute appeared first on Global Publishers.





Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz