Man United Yaitungua Newcastle 4G, Ronaldo Atakataka-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Man United Yaitungua Newcastle 4G, Ronaldo Atakataka-Michezoni leo

TIMU ya Manchester United imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 4-1 dhidi ya Newcastle United, game ambayo imemalizika hivi punde katika Uwanja wa Old Traford na kuwafanya mashabiki wa Man U kutoka vifua mbele huku wakitamba kuwa sasa ni zamu yao ya kunyakuwa Ubingwa wa Uingereza na makombe mengine.

 

Man U walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa Critsiano Ronaldo kunako dakika ya nyongeza ya kipindi cha kwanza (45+2′) baada ya Mason Greenwood kuachia mkwaju uliomshinda kipa wa Newcastle, Freddie Woodman na kuutema kabla ya Ronaldo kuzamisha wavuni.

 

Hii iliamsha furaha kwa Man U kwani mashabiki walitamani Ronaldo afunge bao la kwanza katika mechi hii muhimu kwake ikiwa ni game ya kwanza kwake baada ya kurejea Man U akitokea Juventus, bao ambalo limedumu kwa kipindi cha kwanza cha mchezo huo.

 

Dakika ya Javier Manquillo, akaisawadhishia Newcastle baada ya kupokea pasi kutoka kwa Allan Saint-Maximin wakati wa moja ya counter attack waliyoifanya Nerwcastle.

 

Bao hilo la kusawadhisha liliongeza hasira kwa mashetani wenkundu ambapo dakika ya 62, Cristiano Ronaldo akaiandikia Man U bao la pili baada ya kupokea assist kutoka kwa Luke Shaw.

 

Haikutosha, dakika ya 80 Bruno Fernandes akafanya yake kwa kuiandikia Man U bao la tatu kufuatia assist ya Paul Pogba kabla ya Jesse Lingard kufunga ukurasa wa mabao wa Man U kunako dakika za nyongeza (90+2) akipokea asist ya Paul Pogba.

 

Man U sasa imekaa kileleni mwa Ligi Kuu ya Uingereza ikiwa na pointi 10 mbele ya Manchester yenye pointi 9, Brighton & Hove Albion ni ya tatu ikiwa na pointi 9 na Tottenham Hotspur ni ya nne, nayo ikiwa na pointi 9.

The post Man United Yaitungua Newcastle 4G, Ronaldo Atakataka appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz