Makambo Awaita Mashabiki wa Yanga-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Makambo Awaita Mashabiki wa Yanga-Michezoni leo

KUELEKEA mechi dhidi ya Simba, mshambuliaji wa Yanga, Heritier Ebenezer Makambo, amefunguka kuwa mashabiki wa timu hiyo wanatakiwa kuja kwa wingi kuushuhudia mchezo huo huku akiweka wazi kuwajaza pindi atakapofanikiwa kuifunga Simba.

 

Yanga kesho Jumamosi watakuwa na kibarua kizito cha kumenyana na Simba katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu msimu wa 2021/22 utakaochezwa, Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Makambo alisema kuwa wao kama wachezaji wameshajiandaa kwa ajili ya mchezo huo hivyo kilichobaki ni mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi ili kuwapa hamasa ya kufanikisha ushindi huo huku akiweka wazi kuwajaza mashabiki wa timu hiyo endapo atafanikiwa kuifunga Simba.

 

“Tayari tumeshajiandaa kwa siku kadhaa kukabiliana na Simba katika mchezo wa fainali, kinachotakiwa kwa sasa ni mashabiki kujitokeza kwa wingi ili kutupa nguvu na hamasa kuelekea katika mchezo huu ambapo kama nitafanikiwa kuwafunga Simba basi kama kawaida nitawajaza wana Yanga.

 

“Unajua ni ngumu kutoa ahadi ya kufunga bao kwa kuwa inawezekana kama mchezaji usiwepo katika mipango ya mwalimu lakini yote kwa yote hakuna mchezaji asiyependa kufunga au kufanya vizuri katika mechi muhimu kama hii,” alisema mshambuliaji huyo.

Marco Mzumbe, Dar es Salaam

The post Makambo Awaita Mashabiki wa Yanga appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz