Majina 31 Wachezaji wa Simba Yaliyotumwa CAF-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Majina 31 Wachezaji wa Simba Yaliyotumwa CAF-Michezoni leo

KLABU ya Simba SC imewasilisha majina ya wachezaji 31 waliosajiliwa kwaajili ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu wa 2021/2022 imeelezwa.

 

Klabu hiyo itakayoiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika imepeleka idadi kubwa ya wachezaji waliosajiliwa CAF kwa mara ya kwanza tangu ilipoanza kushiriki michuano hiyo.

 

Kwa upande wa watani zao Yanga SC, imeelezwa kuwa wao wamewasilisha orodha ya wachezaji 28 waliowasajili kwaajili ya michuano hiyo ya Klabu Bingwa Afrika.

 

Wachezaji hao waliosajiliwa kwaajili ya michuano ya Afrika, upande wa walinda lango wapo wanne (4) ambao ni; Aishi Salum Manula, Benno David Kakolanya, Jeremiah Kisubi na Ally Salim.

 

Mabeki ni tisa (9) ambao ni; Erasto Edward Nyoni, nahodha msaidizi Mohammed Hussein Tshabalala, Gadiel Michael, Henock Inonga ‘Varane’, Israel Mwenda, Joash Onyango, Pascal Wawa, Kennedy Juma na Shomari Salum Kapombe.

 

Viungo wapo kumi na tatu (13) ambao ni; Abdulswamad Kassim, Bernard Morrison, Duncan Nyoni, Hassan Dilunga, Jimmyson Mwanuke, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Pape Ousmane Sakho, Peter Banda, Rally Bwalya, Sadio Kanoute, Thadeo Lwanga na Ibrahim Ajibu Migomba.

 

Washambuliaji wenyewe wapo watano (5) ambao ni; Nahodha John Raphael Bocco, Meddie Kagere, Chriss Mugalu, Yusuph Mhilu na Kibu Denis.

The post Majina 31 Wachezaji wa Simba Yaliyotumwa CAF appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz