Majaliwa: Mwakinyo na Kiduku Tunasubiri Wazichape – Video-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Majaliwa: Mwakinyo na Kiduku Tunasubiri Wazichape – Video-Michezoni leo

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema Tanzania inalisubiria kwa hamu pambano la mabondia ambao wamekuwa wakitunishia misuli mara kwa mara, Twaha Kiduku wa Morogoror na Hassan Mwakinyo wa Tanga ambaye kwa sasa ndiye Bondia namba moja Tanzania na Afrika katika uzito wa Super Walter.

 

“Nitumie nafasi hii pia kukipongeza kituo cha matangazo cha Azam (Azam Media) hususan upande wa matangazo ya runinga kwa kuibua na kuutangaza vyema mchezo wa masumbwi nchini, juhudi hizo za Azam Media wakishirikiana na wadau wengine zimewezesha wanamasumbwi wetu kutumia vizuri fursa hiyo kukuza vipaji vyao.

 

“Nimpongeze Twaha Kiduku kwa kumtwanga Dulla Mbabe katika pambano lililovuta hisia za Watanzania wengi, vilevile nimpongeze Bondia Hassan Mwakinyo kwa kumdunda mpinzani wake Mnamibia Julius Indongo kwa TKO na kutetea mkanda wake wa Chama cha Ngumi Afrika (ABU).

 

“Wanamasumbwi wetu wameendelea kuifanya Tanzania itambulike zaidi ulimwenguni sasa tunasubiri pambano la watani Mwakinyo dhidi ya Kiduku,” Waziri Mkuu Majaliwa akiahirisha Mkutano wa nne wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

The post Majaliwa: Mwakinyo na Kiduku Tunasubiri Wazichape – Video appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz