Lwandamina Arudisha Jeshi Lake Kambini-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Lwandamina Arudisha Jeshi Lake Kambini-Michezoni leo

KOCHA Mkuu wa Azam FC, George Lwandamina, baada ya kufanikisha timu hiyo kuvuka hatua ya awali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, jana amerudisha kambini jeshi lake kwa ajili ya kujiandaa na Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2021/22.

Azam imefanikiwa kuiondosha Horseed ya Somalia kwa jumla ya mabao 4-1 katika mchezo wa hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo sasa inakwenda kucheza dhidi ya Pyramid ya Misri.

Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’ alisema: “Timu kwa sasa haipo kambini ila tunatarajia kuanza rasmi kambi yetu kesho (leo) kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya ligi kuu kwa msimu ujao.

“Majeruhi waliopo kwenye kikosi ni wawili tu ambao ni Prince Dube ambaye alifanyiwa upasuaji hivi karibuni na Charles Zulu, ila wengine wote wapo vizuri.”

LEEN ESSAU, DAR

The post Lwandamina Arudisha Jeshi Lake Kambini appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz