LIVE: TANZANIA 1-0 MADAGASCAR – KUFUZU KOMBE LA DUNIA-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

LIVE: TANZANIA 1-0 MADAGASCAR – KUFUZU KOMBE LA DUNIA-Michezoni leo

05’| #KufuzuKombeLaDunia : Beki Erasto Nyoni ameitanguliza Taifa Stars kwa mkwaju wa penati. Nyoni 2’

 

KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Kim Poulsen, amesema Watanzania watarajie ushindi katika mchezo dhidi ya Madagascar unaotarajiwa kupigwa leo Jumanne kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Taifa Stars leo itacheza
mechi yake ya pili ya Kundi J kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2022 dhidi ya Madagascar.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Poulsen alisema: “Timu ipo vizuri kwa ajili ya kupambania ushindi dhidi ya Madagascar hapo kesho (leo).

“Wachezaji wote wapo salama kambini na tayari kwa ajili ya mapambano ili kuhakikisha tunapata alama tatu katika mechi zetu zote za nyumbani.“Tumejipanga vizuri, pia ninafurahishwa na juhudi zinazooneshwa na wachezaji kwani zinanipa matumaini makubwa.

“Tunaenda kushindana na timu ambayo ina uzoefu mkubwa katika michuano mbalimbali, lakini kwa upande wetu sisi tumejipanga kufanya vizuri na Watanzania watarajie ushindi.”Katika mchezo wa kwanza, Taifa Stars ikiwa ugenini ilipata sare ya 1-1 dhidi ya DR Congo.

The post LIVE: TANZANIA 1-0 MADAGASCAR – KUFUZU KOMBE LA DUNIA appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz