Kocha Azam: Kanoute ana Balaa-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Kocha Azam: Kanoute ana Balaa-Michezoni leo

KWA sasa habari ya mjini ni kiungo mkabaji wa Simba, Sadio Kanoute, raia wa Mali, ambaye amefanikiwa kuonyesha kiwango bora kwenye mechi za maandalizi ya msimu ya timu hiyo, ishu hiyo imemuibua kocha wa zamani wa Azam, Ndanda na Lipuli, meja mstaafu Abdul Mingange ambaye amefunguka kuwa kiungo huyo atakuwa tishio msimu huu.

 

Kanoute alionyesha kiwango bora kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya TP Mazembe uliopigwa Jumapili iliyopita licha ya Simba kupoteza kwa bao 1-0 lakini kiungo huyo alionyesha kiwango bora akipoteza pasi nne tu kati ya 39 alizopiga, akifanikiwa kutengeneza utulivu kwenye eneo la kiungo la Simba.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mingange alifunguka: “Nimemuangalia huyu Kanoute ni mchezaji wa viwango vya juu, niwapongeze waliohusika kwenye usajili wake kwani ni mchezaji ambaye anatimiza majukumu yake ipasavyo hivyo namuona mmoja wa wachezaji ambao watafanya vizuri msimu huu, kwani amezoea mazingira kwa haraka tofauti na wachezaji wengine ambao huwa wanashindwa kuonyesha makali kwenye msimu wao wa kwanza wakiwa na timu mpya.”

 

Kikosi cha Simba kinaendelea na maandalizi kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya watani zao Yanga utakaopigwa kesho Jumamosi, kwa Mkapa, Dar.

Hussein Msoleka, Dar es Salaam

The post Kocha Azam: Kanoute ana Balaa appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz