Jembe Jipya Simba Laahidi Makombe-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Jembe Jipya Simba Laahidi Makombe-Michezoni leo

BEKI mpya wa Simba, Mkongomani, Henock Inonga Baka, amewaomba mashabiki wa timu hiyo kumuamini kwa kipindi ambacho atakuwepo hapo, huku akiahidi kutimiza malengo ya timu hiyo ambayo ni kubeba makombe.

Mkongomani huyo amejiunga na Simba msimu huu kwa mkataba wa miaka miwili akitokea DC Motema Pembe ya DR Congo.

Akizungumza na Spoti Xtra, Baka alisema ana mengi ya kuwafanyia Simba, lakini kikubwa anaomba sapoti ya mashabiki huku akifahamu kwamba ni ngumu mchezaji mgeni kuaminika moja kwa moja.

“Nimejiunga na moja ya timu kubwa Afrika ambayo ina wachezaji wengi wakubwa wenye uwezo wa kimataifa.

“Ili mchezaji ufanye vizuri, lazima kwanza uaminike kwa mashabiki, hivyo niwaombe waniamini ili niifanyie makubwa timu yangu mpya ya Simba.

“Nafahamu ushindani uliopo katika timu, hivyo nitahakikisha ninapambana ili kufanikisha malengo ya timu kubeba makombe katika kuelekea msimu ujao,” alisema Baka.

Kaze hana tatizo lolote na viongozi, aliondoka kwa amani baada ya pande mbili kukaa pamoja na kukubaliana kufikia muafaka wa kuusitisha mkataba wake.

WILBERT MOLANDI NA LEEN ESSAU, Dar

 

The post Jembe Jipya Simba Laahidi Makombe appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz