Hitimana Aanza Majukumu Simba-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Hitimana Aanza Majukumu Simba-Michezoni leo

BAADA ya kutambulishwa kuwa Kocha Msaidizi wa Simba, Thierry Hitimana, tayari ameanza majukumu yake mpya katika timu hiyo kwa kuwachimba mkwara mzito wapinzani wao wa jadi, Yanga.

 

Hitimana anatarajiwa kuwa na kibarua cha kuhakikisha Simba inaanza vema msimu wa 2021/22 kwa kushinda mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga itakayochezwa Septemba 25, mwaka huu.

Akizungumza na Spoti Xtra, Hitimana amesema: “Nimeshahudumia timu kubwa, hivyo sina ugeni wowote ingawa itakuwa ni mara yangu ya kwanza kukaa kwenye benchi katika mchezo dhidi Yanga.

 

Nipo hapa kama kocha msaidizi na watu wanatakiwa watambue hilo, hivyo ni wajibu wangu kumshauri mwalimu na yeye ndiyo atakuwa na maamuzi kwa kuwa nipo chini yake. Kuelekea mchezo dhidi ya Yanga, imani yangu ni kwamba tutashinda tu.”

STORI NA IBRAHIM MUSSA NA LEEN ESSAU, Dar es Salaam

The post Hitimana Aanza Majukumu Simba appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz