MSANII chipukizi katika fani ya Muziki, Mavazi na Filamu, Regina Beraldo Kihwele a.k.a (Gynah) anatarajia kutambulisha Kazi zake za Sanaa zenye kubeba jina la "USIKU WA KAHAWA(COFFEE NIGHT)" tarehe 24/09/2021 katika Ukumbi wa Little Theatre jijini Dar Es Salaam.
Katika maonesho hayo kutakuwa na kazi za Uchoraji, ubunifu wa Mavazi, picha za kuchora, pamoja na uzinduzi wa nyimbo zake 5 mpya kwa mashabiki wake.
Aidha, Regina (Gynah) ambaye amesajiliwa na BASATA, ameteuliwa kuwania Tuzo ya Msanii Bora wa Kike (Best Actress) kupitia LIPFF FESTIVAL 2021 Afrika ambapo Tuzo hizo zitafanyika mwishoni mwa mwaka huu 2021 nchini Kenya.
Tuzo hizi zinashindaniwa na Wasanii wengine kutoka Afrika ya Kusini, Cameroon, Uganda, Tanzania na Morocco.

No comments:
Post a Comment