GSM Walibakisha Jembe la Rivers-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

GSM Walibakisha Jembe la Rivers-Michezoni leo

 

HABARI ikufikie kuwa, kiungo mshambuliaji wa Rivers United, Uche Onwuasoanya, huenda akaonekana tena hapa nchini msimu ujao akiwa na uzi wa Yanga.

 

Hiyo ni kutokana na kufuatwa na vigogo wa Yanga hotelini wakimtaka kubaki Dar ili wasaini kandarasi ya awali ya kuichezea timu hiyo.

 

Ndani ya Yanga, wanaokamilisha masuala ya usajili ni wadhamini wao, Kampuni ya GSM ambapo kwa takribani misimu mitatu sasa, kampuni hiyo imekuwa ikisimamia zoezi hilo na kushusha vifaa vya maana.

 

Uche alikuwa ni moja kati ya wachezaji wa Rivers United walioipa ushindi timu yao wa bao 1-0 mbele ya Yanga, wikiendi iliyopita kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali.

 

Spoti Xtra ambalo limebahatika kuwa karibu na kiungo huyo, lilitaka kujiridhisha ukweli wa taarifa hizo kutoka kwa Uche ambaye alikiri kukutana na viongozi wa Yanga muda mfupi baada ya mechi yao kumalizika, juzi Jumapili.

“Ni kweli kuna watu walikuja hapa wakajitambulisha kuwa ni viongozi wa Yanga. Siwezi kusema moja kwa moja nini tumezungumza lakini wameonesha nia ya kunihitaji,” alisema.

Spoti Xtra likamtafuta Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga, Thabity Kandoro ili kujua ukweli wa taarifa hizo ambapo alishindwa kutoa ushirikiano wa moja kwa moja. Uche ni mara ya pili anakuja Tanzania baada ya msimu uliopita kuja akiwa na timu ya Plateau United ambao walicheza na Simba kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

ISSA LIPONDA, Dar

The post GSM Walibakisha Jembe la Rivers appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz