Griezmann Aahidi Makubwa Atletico-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Griezmann Aahidi Makubwa Atletico-Michezoni leo

MSHAMBULIAJI wa Barcelona Antonie Griezmann ambaye amepelekwa Atletico Madrid kwa mkopo, amesema ana furaha kurejea tena Atletico huku akisisitiza kuwa ana uhusiano mzuri na mashabiki wa timu hiyo.

 

Griezimann amekuwa hana furaha kuanzia alipojiunga na Barcelona ambako alishindwa kuendana na mfumo wa klabu hiyo.

 

Hata hivyo, wakati akitua Barcelona mwaka 2019, Griezmann aliwazingua mashabiki wa Atletico waliochukizwa na namna alivyoondoka, lakini sasa anasisitiza kuwa ana uhusiano mzuri na mashabiki hao.

 

“Nafikiri nina uhusiano mzuri sana kati yangu na mashabiki wa Atletico Madrid kwa kuwa nilikaa nao vizuri sana.

 

“Nafikiri nitatoa kila kimoja nilichonacho kwa mashabiki waliopo uwanjani na hata wale wanaotazama kwenye televisheni, lakini ukweli ni kwamba lazima pia nimshukuru kocha Diego Simeone kwa jinsi ambavyo alikuwa akinisimamia kama mwanaye.

 

Amekuwa nguzo muhimu sana kwangu pamoja na familia yangu, nimekuwa nikijisikia vizuri sana kila ninapocheza chini yake,” alisema Mfaransa huyo.

The post Griezmann Aahidi Makubwa Atletico appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz