Gomes Aigomea Namungo-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Gomes Aigomea Namungo-Michezoni leo

WAKATI Simba wakiendelea na kambi ya kujiandaa na msimu mpya wa 2021/22 iliyopo Karatu, Arusha, kocha mkuu wa timu hiyo, Didier Gomes, ameikataa mechi ya kirafiki dhidi ya Namungo, iliyokuwa imepangwa kuchezwa wikiendi hii.

 

Tangu Simba iingie katika kambi hiyo, tayari imecheza mechi moja ya kirafiki dhidi ya Coastal Union mchezo ambao ulimalizika kwa suluhu, huku Gomes akiwa bado ana mpango wa kucheza mechi nyingine za kirafiki, lakini sio dhidi ya Namungo kama ilivyokuwa hapo awali.

 

Chanzo chetu cha ndani kutoka ilipo kambi ya Simba, kilieleza kuwa timu hiyo ilikuwa ina maombi ya mechi tano za kirafiki ikiwa kambini hapo.

 

“Tukiwa huku kambini zilikuwepo timu tano ambazo ziliomba kucheza mechi za kirafiki ambapo tayari tumecheza na Coastal Union, huku zikibakia FC Leopards ya Kenya, Fountain Gate na Mbuni.”

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Mratibu wa Simba, Abbas Ally alisema kuwa: “Timu inaendelea vizuri na mazoezi pamoja na program za kocha ambazo hufanyika mara mbili kwa siku.

 

“Tulipokea maombi ya mechi za kirafiki kutoka kwenye timu tano lakini mpaka sasa tumecheza mmoja dhidi ya Coastal Union.

 

“Mchezo wa kirafiki tuliopanga kucheza dhidi ya Namungo kwa sasa hatuna mpango wa kucheza tena bali tutaangalia maombi ya timu nyingine ambazo tutacheza nazo tukiwa huku.

 

“Lakini pia ifahamike kwamba hatuna mpango wa kuvunja kambi kwa sasa mpaka itakapofika siku yetu ya Simba Day.

MUSA MATEJA NA LEEN ESSAU, Dar

The post Gomes Aigomea Namungo appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz