Gomes Aiandalia Sapraiz Yanga kwa Mkapa-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Gomes Aiandalia Sapraiz Yanga kwa Mkapa-Michezoni leo

KUELEKEA mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga, utakopigwa kesho Jumamosi, benchi la ufundi la Simba chini ya kocha mkuu, Didier Gomes, limepanga kuja na mpango tofauti katika mchezo huo kulinganisha na michezo yao iliyopita, ili kuhakikisha wanaimaliza Yanga.

 

Kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, Simba watakuwa wenyeji wa Yanga katika mchezo wa Ngao ya Jamii, ambapo kikanuni huashiria ufunguzi rasmi wa msimu wa Ligi Kuu Bara.

 

Mara ya mwisho kwa timu hizo kukutana ilikuwa Julai 25, mwaka huu katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC), ambapo Simba waliibuka na ushindi wa bao 1-0.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, kuhusu mchezo dhidi ya Yanga, kocha wa viungo wa Simba, Adel Zrane alisema: “Licha ya kwamba tulipoteza mchezo dhidi ya TP Mazembe. Niwatoe hofu kuwa tayari benchi la ufundi tumekaa chini na kufanyia kazi upungufu ambao tuliuonyesha kwenye mchezo ule, ulikuwa mchezo muhimu kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wetu wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga.

 

“Kupitia mchezo dhidi ya TP Mazembe tumefanya marekebisho kadhaa, na tuna matumaini makubwa ya kushinda dhidi ya Yanga na kutetea taji letu kwani tutakuja kitofauti.”

The post Gomes Aiandalia Sapraiz Yanga kwa Mkapa appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz