Bruno: Tulieni, Ronaldo Anatupa Makombe-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Bruno: Tulieni, Ronaldo Anatupa Makombe-Michezoni leo

KIUNGO wa Manchester United, Bruno Fernandes, amesema ujio wa mshambuliaji Cristiano Ronaldo, kwenye timu hiyo unasogeza makombe karibu.

 

Ronaldo alirejea tena Man United hivi karibuni baada ya kuzitumikia Juventus na Real Madrid kwa mafanikio makubwa.

 

Ronaldo anatarajiwa kucheza mchezo wake wa kwanza na United kesho Jumamosi dhidi ya Newcastle kwenye Premier.

Bruno amesema anaamini kuwa Ronaldo anaweza kumsaidia kocha wa United, Ole Gunnar Solskjaer, kutwaa kombe lake la kwanza kwenye timu hiyo.

 

Fernandes ambaye amekuwa akicheza na supastaa huyo kwenye kikosi cha Ureno, amesema kuwa Ronaldo ambaye amefanikiwa kutwaa jumla ya makombe 33 akiwa na United, Real Madrid na Juventus, atarejesha furaha ya makombe United.


“Kila mmoja anafahamu
uwezo wa Ronaldo, kila mmoja anafahamu kuwa huyu ni mchezaji mkubwa duniani. Nafikiri kwa sasa ni muda wake wa kuisaidia timu hii kutwaa makombe.

 

Tunafahamu ni kitu gani anaweza kutuletea, Ronaldo anachowaza muda mwingi ni kushinda, nafahamu sasa tunakaribia kutwaa ubingwa,” alisema Bruno.

The post Bruno: Tulieni, Ronaldo Anatupa Makombe appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz